Saturday, March 20, 2010

Nenda pole pole..... Serengeti NP

unapokuwa ktk game drive ndani ya hifadhi ya taifa ya Serengeti national park mida ya mchana na ukakutana na kichaka kama hicho juu, ni sharti uende pole pole huku ukiangaza macho vizuri (ikiwezekana hata kwa msaada wa darubini) ili kuona kuna nini chini ya kichaka husika. sehemu kubwa kusini mwa serengeti ni nyasi, hali ambayo inawakosesha wanyama wasiowinda mchana maeneo murua kuuchapa usingizi na kulikwepa jua la mchana. Vichaka kama hivi ni sehemu ambazo mara nyingi utavifuma vitu adimu mida ya mchana...

Timu ya tembeaTz iliwafuma sharubu kadhaa wakiwa wamepumzika ktk kivuli cha hicho kichaka ndani ya Serengeti. Ki ukweli eneo tuliowakuta hawa sharubu hakukuwa na mti hata mmoja karibu. tulipokiona hiki kichaka, kwa uzoefu wake guide wetu alituambia kuwa ktk kichaka hiki lazima tutawakuta sharubu. Na ndivyo ilivyokuwa......

Sharubu mara nyingi hupenda kufanya mawindo yake mida ya usiku. jabo sometimes hata mida ya mchana kama nafasi ikijitokeza huitumia vilivyo kufanya kweli. Mchana hutumika kwa mapumziko.

No comments:

Post a Comment