Saturday, March 27, 2010

Marangu Gate

Mziki wa kupanda mlima kwa kupitia Marangu route huwa unaanzia hapa. Hilo gate ndilo linaashiria kuwa unaingia ndani ya hifadhi ya mlima Kilimanjaro, na kwa wengi huwa ndio mwanzo wa safari itakayokupeleka ktk kilele cha Afrika, Uhuru Peak. Route hii hupendelewa na wengi kwakuwa mpandaji anakuwa anapanda (ascend) taratibu. Hii inaupa mwili nafasi ya kuwenza kuanza kuzoea mazingira taratibu - acclimatisation. hii ina manufaa kwa mpandaji kwani mwili unapoweza kumudu mazingira ya mlimani inakuwa ni kete tosha ya kukuhakikishia kufika Juu kileleni.

Hapo ndio usajili na taratibu zote zinapofanyikia kabla ya kuanza safari.

Ramani inayoionyesha route ya Marangu sambamba na route nyinginezo zote zikiwa zinaelekea Uhuru Peak. Route nyingine zinaelezwa kuwa zinakuwa zina nyanyuka (ascent) haraka hivyo kupelekea mwili wa mpandaji kukosa muda wa kutosha kujirekebisha - acclimatisation.

2 comments:

  1. i'm really proud of you guys, mnaonyesha uelewa mkubwa sana wa maswala mnayopenda ku-share na wenzenu.

    Mungu awajalie maarifa + bidii + upeo mfike mbali zaidi ya kuwa ni blogu.

    one day iwe website ya knowledge ya utalii wa Tanzania. why not?

    ReplyDelete
  2. Shukran sana mdau kwa maneno yenye kututia nguvu. Inatutia moyo wa kuendelea kufanya kazi zaidi na zaidi tupatapo comments kama zako. usisite pia kutuweka sawa pale unapoona mambo hayapo sawa.

    Tunakuomba uifanye tembeatz kuwa moja ya website/blogs unayoitembelea mara kwa mara ktk siku ili upate kujua nini kinaendelea ktk sekta ya utalii hapa nyumbani. Pia wajulishe na wengine kuhusu tembeatz ili nao waweze kunufaika kwa kupata maarifa na uelewa kuhusu maliasili zilizopo ndani ya nchi yetu.

    Juhudi zinaendelea ili kuifanya Tembeatz kuwa source ya kutegemewa ktk habari zinazohusu sekta ya utalii. Keep visiting Tembeatz for more exciting news and photographs

    Ahsante sana

    KK for Tembeatz Team

    ReplyDelete