Saturday, March 27, 2010

Wa Chini; Tarangire - Dec 2009

Desemba mwaka jana Mdau Tom wa Kimasafaris aliwafuma 'wa chini' wakifurahia windo lao la Ngiri. Aliwakuta ndio kwanza wamemwangusha na hata hawajaanza kumla sawasawa.

Taratibu za national parks ambazo zinakataza off-road driving zilimfanya mdau kushindwa kusogea karibu na kupata taswira murua zaidi za shughuli hiyo. Ingelikuwa hili limetokea ktk game reserve, angeweza kusogea karibu.

Ni ktk game reserves ndiko ambako dereva anaruhusiwa kufanya off road driving; kuaiacha barabara na kuingia porini zaidi ili kusogea karibu na walipo wanyama. Ktk National parks off road driving ni kosa ambalo utaweza kupigwa fine takriban $400 ukikutwa na hatia.
Hii ndio sababu serikali inakuwa inahakikisha kuwa nchi inakuwa na game reserve pamoja na national parks. Endapo zote zikiwa national parks, ni dhahiri baadhi ya shughuli ambazo wageni hupenda kufanya zitakuwa zimefikia kikomo. Ahsante ya picha kwa mdau Tom wa Kimasafaris - http://www.kimasafaris.com/

No comments:

Post a Comment