Tuesday, February 9, 2010

Wamekuja kupokea wageni wao

Ndege imetua na una hamu ya kuanza safari yako ya porini, ghafla kabla hujashuka kwenye ndege unakutana na 'wenyeji' wako wamekuja kukupokea. Utathubutu kushuka kwenye ndege? Picha juu ni Simba waliokutwa na Wadau waliofanya ziara yao ndani ya hifadhi ya Ruaha national Park, Iringa.

Picha hii ni ishara inayodhihirisha kwamba wao ndio wako nyumbani na sisi ni wageni wao. hatuna budi kufuata taratibu zao pindi tuwapo ktk mazingira yao. Ruaha national park ni moja ya mbuga kubwa hapa Tanzania na yenye idadi kubwa ya Simba.

Picha juu ni Simba jike watatu wakiwa wamekula pozi karibu kabisa na uwanja wa ndege uliopo ndani ya hifadhi ya taifa ya Ruaha national park. Ahsante ya picha - TTB.

No comments:

Post a Comment