Tuesday, February 9, 2010

Fox Farm : Mufindi, Iringa

Ni Shamba lakini ni sehemu ambayo watu wanaopenda kuachana na purukushani za mijini wanaweza kupata utulivu asilia. Fox Farm lipo Mufindi, nje ya manispaa ya Iringa. Ni sehemu yenye utulivu asilia na tena wa kuvutia. ukiingia hapa ni hakika utazisahau purukushani za mjini na heka heka zake.
Hizo ndio cottages ambazo wageni hutumia kupumzikia.

Sehemu kubwa ya Fox Farm ni malisho ya ng'ombe na farasi na kuna sehemu kuna kijito kidogo kinapita na kuweka mandhari ya hapa kuwa mwanana.


Sehemu wanamokaa Farasi wa Fox farm. kwa mbali ni mto unaopita ndani ya fox farm. Kwa jinsi panavyoonekana, mtu hakawii kubisha kuwa hapa sio TZ na kuanza kujenga hoja ya kuwa pengine ni Swiss au Denmark. Tanzania ni zaidi ya uijuavyo!

Ukiwa hapa, horse riding ni moja ya activity unayoweza kufanya. Wageni wanakuwa na nafasi ya kupanda farasi na kuzungushwa sehemu mbali mbali zilizopo ndani na hata nje ya shamba.

----------------------------------------------------
Kuna mdau alikuwa ameomba kupatiwa Bei na habari zaidi kuhusu Fox Farm, Mufindi.
Kwa yeyote yule ambae atapenda kujua zaidi kuhusu Fox farm awasiliane na Nick - 0784237422. Jina lake lisikutishe, ni mzalendo.

1 comment:

  1. fantastic, tupe bei za accommodation na mengineyo - tusishie kutamani tu.

    ReplyDelete