Bango lililopo ktk gate la Mtemere linakuonyesha ni jinsi gani pori la akiba la Selous lilivyo kubwa. Usishangae mdau kuona kwamba unatembea 125Km ukiwa ndani ya Selous kwenda Tembo Safari Camp bila kutoka nje ya mbuga! Matambwe ndipo yalipo makao makuu ya Selous Game reserve.
Kutokana na ukubwa huu, wageni ambao hupenda kuitembelea Selous kwa undani, hulazimika kufanya Fly camping. Fly camping ni aina ya safari ambayo mgeni hukaa zaidi ya hotel/Camp site au lodge moja anapokuwa mbugani. Fly Camping inatoa fursa kwa mgeni kutumia muda mwingi kutembelea eneo na kupunguza muda wa safari za kwenda mbugani na kurudi hotelini. sambamba na hiyo, fly camping inakuweka karibu zaidi na maeneo yenye vivutio ulivyovifuata.
Kwa kuwa Selous sio National park, usimamizi na uendeshwaji wake upo chini ya idara ya wanyama pori (wizara ya maliasili na Utalii). Ndio maana hata ukienda tovuti ya TANAPA, Selous pamoja na game reserves nyinginezo hazipo listed huko. Viingilio vya kuingia Game reserves ni tofauti na vya kuingilia National Parks.

No comments:
Post a Comment