Friday, February 12, 2010

Ngoitoktok - Ngorongoro crater

wadau wengi wanaotembelea Ngorongoro crater hupita hapa kwa ajili ya kupata lunch wakati wa mchana. ni sehemu maarufu sana kwa wageni wengi wanaotembelea crater kuja kupata maakuli yao. Kinachowavuta wengi ktk hii picnic site ni utulivu na mandhari nzuri ya eneo hili.

Jambo moja ambalo lazima utaambiwa na guide wako ni kwamba usithubutu kula/kushika chakula chako ukiwa nje ya gari au sehemu ya wazi. hapa kuna vipanga (mwewe) ambao wanafanya dive ambazo hizijawahi shuhudiwa sehemu nyingine. wana shabaha ajabu, ukikaa vibaya, jua lunch yako watabeba na utatoka patupu.

Ukimaliza lunch yako ndio unaweza shuka nje ya gari na kuanza kukagua. Ukipaangalia unaweza ukasema vipanga hao wanaonewa lakini wanapotokea hujui utashangaa huna chakula chako. ndio baadhi ya adventure ndani ya ngorongoro crater.

No comments:

Post a Comment