Sunday, February 7, 2010

Ruaha River Lodge

Ruaha River Lodge ni moja ya hoteli zilizopo ndani ya Hifadhi ya taifa ya Ruaha National Park. hoteli hii ipo kando kando ya mto Ruaha ambao unakatiza ndani ya hifadhi hii murua.

Kuwepo kando kando ya Mto Ruaha, kunakupa mgeni nafasi murua na ya uhakika ya kujionea wanyama wengi waishio ndani ya Hifadhi hii kipindi chote cha mwaka. hii inatokana na ukweli ya kwamba kipindi cha masika, mto ruaha ndio huwa chanzo muhimu cha maji wa wanyawama hawa. hii inakupa uhakika wa kuona wanyam wengi ukiwa ndani ya hifadhi. Picha juu ni muonekano wa mti Ruaha tokea kwenye moja ya vyumba vya hoteli hii. Japo ilikuwa ni kipindi cha kiangazi lakini mandhari yake bado ina mvuto. picha hizi zilipigwa na mdau Tom wa Kima Safaris alipokuwa huko mwaka jana.

Mahali ilipo hotel hii (pembezoni mwa mto Ruaha) inakupa nafasi nzuri ya kujionea mandhari ya hifadhi ukiwa ktk Balcony ya chumba chako. Mandhari inavutia kiasi cha mtu kutaka kumalizia safari yako chumbani na kurudi ulipotoka. Ruaha national Park ipo takriban 120km toka Iringa mjini, ni moja ya mbuga kubwa Tanzania yenye vivutio vingi vya kuona na kujifunza.

Photo framing. Ni balcony ya moja ya vyumba ambavyo vipoRuaha River lodge. Licha ya ukame uliokuwapo kipindi hicho, bado muoneka unavutia vilivyo.

Moja ya vyumba vya Ruaha River Lodge kinavyoonekana kwa nje. Utaratibu ni ule ule, Hotel zilizopo ndani ya hifadhi hazina uzio, hivyo hapo kilipo chumba kimo ndani ya hafidha kwa asilimia mia moja. Jua likizama lazima uombe escort ya askari mwenye silaha kama unataka kutoka nje mida ya usiku.

Tembo akivinjari pembezoni mwa mto Ruaha, mbele ya Ruaha river lodge.

Kuna tofauti kubwa sana kati ya mtu kukaa ndani au nje ya Hifadhi. Unapokaa ktk hoteli iliyo nje ya Hifadhi (karibu na mipaka wa hifadhi), kwa kiasi kikubwa mazingira yake yatakuwa hayatofautiani sana na yale ya nyumbani kwako ulikokuacha. Sambamba na hii, unakuwa upo mbali na wanyama ambao umesafiri kilometa nyingi kuja kuwaona na kuwafurahia.

Unapoamua kutembelea mbuga au hifadhi, jaribu kufanya mpango walau usiku mmoja upate kulala ktk hotel iliyopo ndani ya Hifadhi. kama una moyo (kama kikosi cha Tembea) fanya tented Camping ktk camping sites au la kama roho nyepesi basi lala ktk hotel ya kawaida.

Unapolala ndani ya hifadhi, moja ya vitu vitakavyokusisimua (ukibahatika), ni milio ya wanyama mbalimbali ambayo utakuwa ukiisikia mida ya usiku. Hii ni hali ya kawaida usiku kwani sauti huwa inasafiri umbali mrefu usiku kushinda mchana.

Hapo utaweza kumsikia bwana Afya (fisi) akiwa kwenye mishemishe zake za kuzengea mawindo ya wenzie au mizoga waliyoiacha. kama ukiwa karibu na mto au bwawa basi Viboko nao utawasikia bila wasi wasi, masikio (Tembo) nao utawasikia wakitoa milio yao mida ya usiku. Na hata Sharubu pia kwa mbali au hata kwa karibu. Sambamba na milio ya wanyama wakubwa, milio ya ndege mbalimbali nayo huwa haikosekani.

Milio hii ya wanyama sio kitu ambacho tumekizoea ktk maisha yeti ya kila siku hali ambayo itakupa msisimko wa kipekee na kuifanya safari yako ya porini kudumu akilini mwako muda mrefu na kukufanya utake kurudi porini tena na tena.

Wengi huingia porini kwa lengo la kuona wanyama, lakini kuna mengi mengineyo ya kujifunza kuhusu wanyama na mazingira yao. na baadhi ya haya mambo unapata fursa ya kujifunza na kuyajua pindi unapokuwa karibu na wanyama ktk vipindi tofauti tofauti (Usiku na mchana).

Ndani ya Hifadhi ya Ruaha kuna sehemu nyingi za malazi, Ruaha river lodge ni mojawapo. kama unapenda camping basi kuna camping sites kadhaa baadhi nyingne zikiwa kando kando ya mto ruaha. tented camping ni njia mojawapo ya kukusogeza karibu kabisa na wanyama. ktk yote haya hakikisha unayafanya ukiwa na guide mwenye uelewa au wewe mwenye uwe na uelewa mkubwa na mambo ya porini na wanyama pori.

No comments:

Post a Comment