Saturday, February 6, 2010

Mombo mpaka himo

Baadhi ya Taswira za kipande kati ya Mombo hadi Himo-njia panda. Ni moja ya sehemu ambazo zina mandhari nzuri sana ktk safari ya kuelekea Moshi au Arusha. Picha hizi zilipigwa mnamo mwezi December mwaka jana.

Milima ya Usambara.
Kupanda kwa matumizi ya plastick ni moja ya mambo yaliyopelekea zao la Mkonge kuyumba ktk soko. vitu vingi ambavyo awali vilikuwa vikitengenezwa kwa bidhaa zitokanazo na zao la mkonge sasa hivi vinatengenezwa kwa kutumia plastic. Licha ya hali hiyo, yapo mashamba machache ambayo yanaendelea na kilimo cha mkonge ktk mikoa ya Tanga na Morogoro.

Unapoimaliza milima ya Usambara, unaanza milima ya Wapare. Japo haina jina rasmi, lakini ki-jiografia ni muendelezo wa Milima ya Usambara (Usambara Ranges). Kwa wale wenzangu na mie tuliosoma mtaala wa Taasisi ya Elimu ktk shule za msingi za Halmashauri, tutakumbuka kusoma habari ya milima ya Usambara.

Milima ya Upareni ikiendelea kukusindikiza ukiwa njiani kuelekea Himo njia panda. hapa ukiwa unakaribia kufika Mwanga - Stand.
Mwanga ikiwa inaonekana kwa mbali, kulia.


Hapa ukiwa unakaribia kufika himo, Kwa mbali ni Mlima Kilimanjaro ambao kama kawaida yake huwa unakuwa umefinikwa na mawingu kwa kipindi kirefu cha siku. unaweza ukakaa moshi siku mbili na usiweze kuona kilele cha mlima huu kwa kuwa huwa unafunikwa na mawingu kwa muda mrefu. hali ndio huwa mbaya zaidi kipindi cha mvua. unaweza bisha kuwa hapa hakuna mlima.

kuna siku moja nilikuwa njiani na swahiba wangu tukielekea Bukoba kupitia Nairobi - Kampala. Safari hii ilikuwa na partly adventure, partly ki jamii. kwa Bahati mbaya, Bus tulilokuwa tukisafiria, liliharibika pale Himo wakati likikaa ktk foleni ya kuingia ktk mzani. Kutokana na kuwa lilikuwa ni model mpya kwa kipindi kile (2007), spea ya kifaa kilichopata hitilafu haikuweza kupatikana haraka Moshi, Arusha na hata Dar. Ikabidi kiagizwe toka Kwa watani wa jadi. Hali hii ilipelekea sisi abiria tukae himo zaidi ya masaa 24 tukisubiri basi litengemae ili tuendelee na safari yetu ambayo bado ilikuwa ndefu - Kumbuka hapo inabidi tufike Nairobi, Then tuitafute Busiya (mpaka wa Unganda na Kenya) then tuitafute Kampala. ukiimaliza Kampala kuna kipande mpaka uupate mpaka wa Mtukula.

Swahiba wangu alikuwa ni mara yake ya kwanza kufika Moshi, na alikuwa na hamu sana ya kuuona Mlima. Tukiwa njiani nikamhakikishia kwamba tukifika Himo njia panda mlima utauona kirahisi. akajenga imani na matumaini.
Kwa kipindi chote tulichokaa Himo tukisubiri spare ya bus ije nilikuwa na wakati mgumu kumshawishi swahiba wangu kwamba mlima auonao ni Kilimanjaro licha ya kwamba kilele chenye theluji hakionekani. Hakukubaliana nami hata kidogo huku akisisitiza ya kwamba hatakubaliana nami mpaka atakapoona kilele chenye barafu.

Ilibidi niombe msaada toka kwa wenyeji tuliojenga nao urafiki kwa kipidni tulichokaa pale himo ili wanisaidie ktk ubihshi huu kwani theluji ilikuwa haionekani hata kidogo kutokana na kuzingirwa na mawingu muda wote kwa muda mrefu.
Mwisho wa siku nilikubali kushindwa kwani mawingu yalificha theluji kwa siku zote tulizokaa himo njia panda. Namshukuru mungu sikuweka dau maana ningepoteza dau langu.

No comments:

Post a Comment