Monday, February 1, 2010

nyama ni msosi kwao....

Waswahili tuna msemo wa kwamba Simba akizidiwa, hula nyama. Hali inakuwa tofauti kudogo kwa ngedere kwani yeye nyama ni sehemu ya menu yake. Ngedere hula nyama, majani na matunda sambamba.

Ktk tukio hili tulimkuta ngedere akiendelea kumtafuna Swala mtoto aliyemkamata wakati wa kila. hii hali hutokea sana kwa ngedere ktk kipindi cha kiangazi ambacho majani na matunda yanakuwa adimu porini. mama swala hakuwa mbali akishuhudia mwanae akigeuzwa kitoweo na ngedere huku yeye akishindwa na kula kufanya ili kumuokoa mwanae.

Jamaa akiendelea kupata lunch yake ya swala mtoto

Wengi wetu tulisikitishwa na kitendo cha ngedere huyo hasa hasa kwa kumuona Mama Swala akishuhudia mwanae akitafunwa na ngedere. lakini ki ukweli hii ndio system ya porini. hivyo ndivyo wanyama wanavyoishi na kustawi porini.
hali ya jamii moja kula wanyama wengine ni muhimu sana ili kuweza kubalance neema ktk eneo husika. ukiondoa wanyama wanaokula wanyama wenzao, basi haitachukua muda mrefu wanyama wanaokula nyasi watakuwa ktk hali mbaya sana. hii inatokana na ukweli kwamba watazaliana sana kiasi cha mazingira kushindwa kuweza kuwa support kwa malisho bora. hivyo hali hii inakuwa ni tishio kubwa kwa mazingira.
hali inakuwa hivyo hivyo ambapo wala nyasi wanapotoweka, mbuga inageuka kuwa pori na kufanya wanyama wadogo wadogo kushindwa kumudu mazingira. kwa wenye uwezo watakimbilia mbali kwa wasio na uwezo huweza kufa na kutoweka kabisa.

hivi ndivyo equation ya nature inavyo ji-balance yenyewe.

No comments:

Post a Comment