Monday, February 1, 2010

Mufindi: haivumi lakini imo.....

Mufindi imekuwa maarufu kwa kilimo cha chai. wengi wetu tuliosoma shule za Halmashauri tulisoma habari za kilimo cha chai Mufindi. picha juu ni ushahidi tosha kwamba wananchi wa mufindi wanaendeleza libeneke la kilimo cha chai. Lakini mtundiko huu unakuonyesha zaidi ya kilimo cha chai, kwani Mufindi kuna mandhari tulivu na zenye kuzutia kiasi cha kwamba ukionyeshwa unaweza sema hapa ni Uswiss au sehemu nyingine bara Ulaya.

Hali ya hewa ya Mufindi huvutia ndege wengi ambao hawapatikani sehemu nyingine kufanya makazi yao ndani ya Mufindi.


Hili ni moja ya mabwawa yanayopatikana huko Mufindi ambapo wageni hupata fursa ya kuangalia mandhari ya miti na ndege wakati wakiwa katika mtumbwi - canoe.

Mime aina ye Fern nayo ipo ya ku mwaga.

No further comment on the photo above; naandika kiingereza ili kuonyesha msisitizo

Wananchi wakiendelea na shughuli zao za kilimo cha chai.

Mdau Tom wa Kima Safaris alifanya ziara mnamo mwaka jana mwishoni na kutumwagia taswira hizi maridhawa za maeneo mbali mbali huko wilayani mufindi. Kiukweli mandhari ya huku ni tulivu na yenye kuvutia. Ukitia mguu huku ni dhahiri shida na matatizo ya duni utaviweka kando na kufurahia mandhari tulivu ya huku. Kunafikika kirahisi ktk vipindi vyote vya mwaka.

1 comment:

  1. fantastic, iringa bab kubwa!

    mazingira shwari kabisa hayo, unatakiwa kuwa na taste ya mambo mazuri ku-appreciate maisha ya countryside kama hayo.

    wabongo wanavyopenda kelele za mjini wanakuona mshamba ukizungumzia country life.

    ReplyDelete