Sunday, February 7, 2010

Mto wa Mbu

Mto wa Mbu ni moja ya vitongoji ambavyo utavipita kama unaelekea Hifadhi za Manyara, Ngorongoro, Serengeti na kwengineko. Hii sehemu ipo ndani ya Bonde la Ufa na karaibu kabisa na hifadhi ya Taifa ya Manyara National park. Baadhi ya wageni wanaotembelea hifadhi ya Manyara, huwa wanalala Mto wa mbu. Kuna hotel na camp site kadhaa.

Barabara ya Lami uionayo inaishia unapoanza kuingia ndani ya eneo la hifadhi ya Ngorongoro. ni mkeka kwa kwenda mbele.

Uwepo wa eneo hili karibu na hifadhi ya Manyara na kuwa kando kando ya barabara iendayo ktk vivutio vikubwa vya utalii ktk taifa letu kunaleta hamasa ktk eneo hili. Ujenzi wa sehemu za biashara unaendelea kila kona huku kila mwekezaji (wazalendo) wakilenga huduma zinazoranda na sekta ya utalii. Wafanyakazi wengi wa hoteli zilizopo Manyara, hufanya Mto wa mbu kuwa eneo lao la makazi.

Nilijitahidi sana kuangaza macho kila kona ili niuone huo mto wa mbu lakini sikuambulia kitu zaidi ya mashamba ya mpunga yaliyoshamiri eneo hili. Wakazi wa hapa ni wakulima wazuri wa mchele ktk mkoa wa Arusha.

Miundo mbinu imetulia

No comments:

Post a Comment