Monday, February 8, 2010

Kwato zao

Kuna namna nyingi ambazo mgeni anaweza kujionea mambo ktk mbuga au hifadhi aliyotembelea. Njia hizo ni Kutembea kwa kutumia motokaa, Boti, Miguu, mapulizo ya Moto au Micro light aircrafts. Game walk aka Makanyagio ni moja ya namna ambayo itakuweka karibu sana na wanyama na hasa hasa mazingira yao. Game walks zinapofanywa, ni lazima mgeni awe ameambatana na guide mwenye silaha kwa sababu za kiusalama. Japo kiukweli silaha kubwa anayokuwa anajihami nayo ni uelewa na uzoefu wake wa wanyama pori na mazingira yao. Silaha huwa inabebwa kwa kukupa motisha wewe mgeni.

Uwepo wako wa karibu na mazingira unakuwezesha wewe mgeni kuona mambo mengi ambayo usingeweza kuyaona uwapo ktk gari au namna nyingine za kutembelea hifadhi. kwa makanyagio, unaweza kuona jinsi wanyama wanavyofuata njia hizo hizo kila siku ktk mizunguko yao kama vile sisi binadamu tufanyavyo.
Pia unaweza jionea jinsi baadhi ya wanyama wanavyoweka alama zao za kuwaongoza ktk safari zao. Kiboko huwa na tabia ya kutawanya kinyesi ktk mapito yake ili kuweka alama za kumsaidia kujua njia.

utapata fursa ya kuona jinsi kwato za wanyama mbali mbali zinavyotofautiana kama ilivyo ktk picha za hapo juu. picha ya kwanza ni kwato za swala wakati picha ya pili ni Kwato za Kiboko. picha zote zimepigwa na mdau Tom alipotembelea Hifadhi ya Ruaha national park

No comments:

Post a Comment