Wednesday, February 3, 2010

Mbuyu mchanga

Ktk Mtundiko wa Hata mbuyu huanza kama mchicha, kuna mdau alisema kuwa hajawahi kuuona mti mbuyu ukiwa mdogo aka mchanga. ktk pita pita zangu, nilipita mahali ambapo mbegu za ubuyu zilikuwa zimemwagwa na baadhi ya hizo mbegu zilianza kuchipua.
Japo nilibahatika kuuona na kuupiga picha mbuyu huo, bado nakubaliana na jambo la mchangiaji kwamba kiukweli sijawahi kuuona mbuyu ambao upo rika la teenager.

Mvua zikinyesha, mbegu za mbuyu zilizozagaa huchipua kama taswira zionyeshavyo juu. lakini jua likishika hatamu zinapotoa, hii ni hali ya hapa mjini. Lakini ktk pita pita zangu nje ya jiji au hata maeneo ya mashambani, mibuyu ninayokutana nayo ni mikubwa.

Hii ni changamoto kwenu wadau, kwa yoyote yule mwenye taswira ya mbuyu teenager aturushie ili tuuone.

No comments:

Post a Comment