Wednesday, February 3, 2010

Mabaki yana nafasi ktk mfumo wa maisha ndani ya Hifadhi

Moja ya sheria unazotakiwa kuzingatia mgeni ukiwa mbugani ni kutokuokota kitu chochote (au mabaki ya mnyama) pindi unapokuwa ndani ya mbuga au hifadhi. Kwa haraka haraka unaweza usielewe nia na madhumuni lakini ukikutana na hali kama hiyo hapo juu aliyokutana nayo Mdau mwenzetu utaelewa ni kwanini.

Mnyama anapokufa, kwanza kabisa hiyo huwa ni neema kwa wale wanaokula wanyama wengine. baada ya kundi hilo kupata chao, hufuata kundi la wale wazee wa mizoga - Fisi na ndege tai. wao nao huchukua share yao na kuacha kila ambacho kimewashinda.
Baada ya hapo sasa, mabaki hayo huendelea kusopport maisha ya viumbe hai wengine kwa namna mbali mbali. Mathalan, kipindi cha mvua, baadhi ya wadudu hufanya makazi yao ndani ya mabaki ya wanyama. huyatumia kujikinga na mvua na hata kuyafanya sehemu ya kutagia mayai au kuzaliana.

Kutokana na hali hii, ndio maana mamlaka zinazosimamia maeneo haya zinakataza kabisa kitendo cha mgeni kuokota mabaki ya wanyama unayokutana nayo. kwani kwa kufanya hivyo, unaharibu mazingira au makazi ya viumbe hai wengine ambao nao ni muhimu ktk mustakabali wa eneo husika. Ukiangali hilo fuvu la nyati (kwenye pembe) utaona kuna vitu vinaota, hiyo ni dalili ya kwamba fuvu hilo linaendelea ku-support maisha ya viumbe hai wengine hapo lilipo.

Ni muhimu tukaelewa hizi taratibu ili kuhakikisha kuwa mbuga na hifadhi zetu zinadumu kwa miaka mingi.

No comments:

Post a Comment