Monday, February 15, 2010

Kipupwe na ukungu wa Arusha

Kwa jinsi joto linavyotutesa hapa jijini kipindi hiki, taswira kama hizi zinazoashiria hali ya ubaridi ndani ya A-city zinakuwa na mvuto wa kipekee katika fikra za wengi hususan wale ambao tumewahi fika Arusha. Ukungu unakuwa unatanda sehemu kubwa. Hii ni barabara kuu ya Moshi - Arusha

Mida ya asubuhi, ukungu huwa unakuwa umetanda barabarani hasa katika kipindi cha baridi. picha hizi zilipigwa mwezi December 2008.


Hiyo ndio Naura Springs Hotel. Ipo karibu na AICC.

Ukiingia mitaa ya kati nako kiwingu cha uvivu kilikuwa kimetanda pia. Kwa jinsi hali ya hewa hapa Dar ilivyo sasa hivi, unatamani sana aidha uhamie Arusha (jambo ambalo lina ugumu wake) au Ufanye transfer ya hali ya hewa ya Arusha ihamie huku (jambo ambalo litaishia kuwa la kusadidikika). Acha tu Arusha iitwe Geneva of Africa, jiji hili lina mengi ya kuvutia na kukuburudisha kimwili na kiakili.

No comments:

Post a Comment