Moja ya tawira zilizokuwa zinatumika enzi hizo kuelezea bonde la ufa ktk somo la Jiografia ni taswira ambayo imerandana na hii. Ilikuwa inapatikana ktk atlas tulizokuwa tukizitumia shule ya msingi. Jengo unaloliona kwenye ukingo wa bonde la ufa ni Lake manyara wildlife lodge.
Unapokuwa anaelekea Ngorongoro au Karatu utapita eneo lijulikanalo kama view point. hapa utapata fursa ya kujionea Bonde la ufa na Hifadhi ya Manyara.Sehemu kubwa ya Manyara NP ni msitu mnene huku sehemu iliyobakia inachukuliwa na ziwa manyara lenyewe na sehem ya wazi kidogo. Ni hifadhi ya kipekee kwa Tanzania kwani hifadhi nyingine nyingi ni vichaka vya nyasi fupi au nyasi mwanzo hadi mwisho (Serengeti). Ziwa linaloonekana kwa mbali ni Ziwa Manyara.
No comments:
Post a Comment