Wednesday, February 3, 2010

Itakulazimu uwe mdogo.....

Uko ktk misele yako porini mara unakutana na jamaa wametanda barabarani kama jinsi mdau alivyokutana nao akiwa ndani ya Hifadhi ya taifa ya Manyara National park. Hapo ndugu yangu lazima uwe mdogo na wala usijaribu kutumia mbinu za usalama barabarani ulizo fundishwa driving school au ulizoziona ktk kipindi cha luninga cha usalama barabarani cha BP. Kelele ni mwiko kwa hawa jamaa.

Waache wafanye shughuli zao huku wewe ukiwa mtazamaji, after all wewe ndio umewafuata huko ili kuwaangalia wakiendelea na shughuli zao za kila siku, so Enjoy the show!

Dereva ukiwa porini huruhusiwi kabisa kupiga honi au hata kupiga muziki kwa sauti ya juu. Hii ni moja ya taratibu ambazo mgeni anapashwa kuzingatia awapo porini. Sababu kuu ya kuwepo kwa hii taratibu ni kukulinda mgeni dhidi ya wanyama kama tembo ambao kelele ya honi ni kero kubwa kwao. Honi inaweza kumfanya tembo abadili mwelekeo wa shughuli zake na kuanza kufanya mambo sivyo ndivyo. Ni sheria muhimu na kuizingati uwapo porini mwenyewe, hasa kama hauna guide anayezielewa vilivyo taratibu hizi. Baadhi ya sheria na taratibu za barabarani huku za uraiani hazipo applicable mbugani.
Tembea Tz itakuwa inakupo dondoo ya baadhi ya hizi taratibu ili safari yako ya porini iwe salama na yenye manufaa kwako, endelea kutembelea tembeaTz kwa dondoo zaidi.

No comments:

Post a Comment