Monday, February 15, 2010

Binadamu na wanyama pori - side by side

Wengi tumezoea kwamba wanapoishi wanyama pori, basi Binadamu anatakiwa kuishi mbali napo. Hali ni tofauti kidogo na jinsi TembeaTz ilivyoshuhudia mambo ndani ya Arusha National Park. Unapokuwa upo pembezoni mwa Lake Momella (Kubwa) utaweza kujionea nyumba kadhaa na shughuli za kilimo zikiendelea pembezoni kabisa mwa hifadhi. Hizi ni nyumba zilizopo ndani ya eneo linalojulikana kama Majani ya Chai huko Arusha, Nje ya eneo la hifadhi.

Picha juu inakuonyesha sehemu ya uzio uliowekwa kutenganisha eneo la hifadhi na eneo la kijiji - makazi. Ziwa unaloliona mbele ni Momella Kubwa na flamingo wakijivinjari ndani yake. Maji ya ziwa hili ni Alakaline, hayafai kwa matumizi ya kawaida ya binadamu.
Hapa wananchi wanaishi na kulinda vivutio hivi. Yawezekana kabisa ni kutokana na juhudi za kuwaelimisha na pia kuwaletea maendeleo kutokana na jamii zao kunufaika na mapato yanayotokana na hifadhi.

No comments:

Post a Comment