Wednesday, January 20, 2010

Wanaijua mipaka ya hifadhi kinamna


Wanyama wa porini, kwa namna fulani wanaelewa mipaka kati ya Mbuga/hifadhi na nje ya hifadhi. hii hutokana na shughuli ambazo zinafanywa nje ya hifadhi, kuwa tofauti sana na hali ilivyo ktk eneo linalohifadhiwa.

Endapo hifadhi itakuwa imezungukwa sana na shughuli za binadamu, na kibaya zaidi binadamu hao watakuwa wana wawinda au kuwatega na kisha kuwaua wanyama kwa wingi, basi wanyama hujenga mazingira ya kutopita au kwenda kabisa eneo lile na badala yake kuendelea kubaki ndani ya mbuga. Lakini endapo jamii inayozunguka pori ina uelewa mzuri wa kuhifadhi wanyama na kutowabugudhi, basi baadhi ya wanyama huwa na tabia ya kupita, japo misele yao huwa wanaifanya usiku.

Niliwahi kumuuliza game ranger mmoja kuhusu hii hali huko Mtemere selous na akanieleza kuwa wanyama wanajua maeneo salama. Moja ya mambo aliyonieleza ni kuwa ifikapo usiku, Wanyama wengi hukusanyika katika eneo karibu na gate la mtemere na kulala hapo. "Ukifika usiku hapa utakuta kuna kundi kubwa la swala, Tembo, Jamii ya nyani na wanyama wengine wala nyasi".
hii ni kutokana na uwepo wa ranger muda wote ktk gate la Mtemere, hali ambayo wanaichukulia kuwa ni hali ya usalama kwao.

No comments:

Post a Comment