Wednesday, January 20, 2010

Hoteli zilizopo ndani ya hifadhi hazina uzio

Ili safari yako ya porini iwe ya raha na salama, ni vizuri ukielewa kwamba kama utakaa ktk hoteli ambayo ipo ndani ya hifadhi, Jua ya kwamba hapo ulipo hakuna fence inayozmuia mnyama kufika mlangoni kwako. Hii inatokana na sheria na taratibu za ujenzi wa hoteli au majengo ndani ya hifadhi. Ujenzi wa uzio hupelekea kuziba au kuvuruga mapito ya wanyama, jambo ambalo mamlaka zinazosimamia hifadhi hazitaki kutokea. hivyo basi, ili hoteli iweze kujengwa na wanyama wasiharibiwe mapito yao, ni lazima hoteli husika ijengwe bila ya kuwa na uzio.

Uwapo ndani ya chumba chako unaweza kuhesabu upo ndani, lakini ukikanyaga nje, jua ya kwamba tayari upo ktk sehemu ya ecosystem ya mbuga.

Ukipita mida ya usiku unaweza bahatika kuwaona Swala au digidigi wakila majani pembeni kabisa ya pavement unayotembea. Mchana panakuwa tulivu kwani wanakuwa wanaenda mbali.


Moja ya majengo (vyumba) vilivyopo ktk hoteli ya Serena Serengeti.

Ifikapo usiku (jua likishazama), mgeni hupewa maelekezo ya kupiga simu reception na kuomba escrot. Escort hiyo huwa ni mlinzi ambae atagonga chumbani kwako na kukupeleka kule utakako, kama ni restaurant au bar. Mlinzi huwa na tochi na bunduki.

Sehemu ya mbuga ya Serengeti kama inavyooneka ukiwa mbele ya bwawa la kuogelea lilipo Serena Serengeti lodge.

Mongoose wakiranda randa karibu na restaurant ya Serena Serengeti hotel. Hawa wanapatikana mitaa hii muda mwingi.

Uelewa wa mazingira uliopo na taratibu zake zitakusaidia wewe kama mgeni kufarahia safari yako na kukuhakishia usalama wako pia. mgeni unapofika ktk hizi hoteli huwa unapewa maelekezo ya nini ufanye ili kukaa mbali na shari. ni vyema ukitoa ushirikiano kwa kufuata maelekezo utakayopewa.
Yaweza onekana kama ni hali ya kutisha lakini hii hali ya kuwa katika eneo ambalo muda wowote unaweza kuonana na mnyama wa porini huwa na msisimko wa kipekee kwako. Utashangaa sasa pale utakapokaa ktk hoteli iliyopo nje ya mbuga (lakini karibu na mpaka), huwa mara nyingi hazina uzio ili kuruhusu wanyama waweze kuranda randa na kuwaburudisha wageni.

hali hii ipo pia hata kwa Camping sites, nazo pia hazina uzio wa aina yoyote. huko sasa malazi ni kwenye camping tent.

1 comment:

  1. NIMEZIPENDA HIZO PICHA NA PIA NIMEYAPENDA MAELEZO YAKE.
    SAFI SANA

    GEORGE BUNDALA

    ReplyDelete