Tuesday, January 19, 2010

Ndege zina namba ya usajili pia.. si vibaya ukijua

Namba ya usajili ya ndege ina mfumo sambamba na namba za usajili wa vyombo vingine vya usafiri wa ardhini. Mfumo huo huutambilisha nchi ndege inayotoka na herufi au alama pekee ya ndege hiyo. Picha juu ni ndege inayomilikiwa na coastal aviation ikiwa na namba za usajili 5H-POA. 5H ni country code ya Tanzania, wakati POA ni alama inayoitambulisha ndege husika. mmiliki wa ndege yuko huru kuweka herufi zozote baada ya country code, ili mradi kusiwe na ndege nyingine yenye alama kama hiyo.
5H-TZT (TanzanAir) na 5H-CCT (Coastal Aviation) zikiwa zimeegesha JNKIA, Terminal One- Airport ya zamani

5H-BMP (regional Air) ikiwa inaegesha Arusha Airport.

5H-MAY (Zan Air) ikiwa inasubiri kula vichwa Zanzibar Airport

Hata Hot Air balloons nazo zinakuwa na namba yausajili ambayo mfumo wake uko sawa sawa na ndege za kawaida za abiria na mizigo. kwa hapa Tanzania ni ndani ya mbuga ya Serengeti pekee ambako unakutana na safari za haya mapulizo ya moto. kampuni ya Serengeti balloon safaris ndio yenye leseni ya kuendesha biashara hii.

ndege ni moja ya nyenzo muhimu inayokuwezesha kusafiri haraka. japo safari ya ardhini inakupa nafasi ya kuona mengi mengineyo uwapo njiani, lakini usafiri wa ardhini una mipaka yake. kwa yule ambae hana muda mwingi wa kutumia ktk safari na fungu lake linaruhusu basi ndege ni moja ya option anayoweza chukua endapo atokako na aendako ndege za abiria zinafanya safari.

TembeaTz inaamini kwa kukupa dondoo hizi, ni dhahiri siku nyingine ukiiona ndege mahali hautaiangalia juu juu bali utajaribu kudadisi ili kujua namba yake ya usajili ni ipi. bofya hapa kupata dondoo zaidi kuhusu namba za usajili wa ndege ktk ngazi ya kimataifa.

No comments:

Post a Comment