Wednesday, January 13, 2010

Wakoloni walichapana ndani ya mbuga ya Selous

Vita ni Vita....., jamaa baada ya kuona kichapo kinakuwa kikali akaamua kutia mpira kwapani na kuangalia ustaarabu mwingine

Kupatikana kwa mabaki ya silaha na vifaa vya kivita ndani ya pori la akiba la Selous ni moja ya uthibitisho kwamba enzi za ukoloni, Selous Game reserve ulikuwa ni uwanja wa mapambano. Inaelezwa kwamba Wajerumani na Waingereza walipambana ndani ya Mbuga hii wakati wa vita ya kwanza ya Dunia. Picha juu ni mabakii ya Steam engine ambayo inaelezwa kuwa ilikuwa mali ya Wajerumani wakati wa mpambano.

Ukienda Selous utajifunza mengi mengineyo ukiachia wanyama wa porini waliopo ndani ya pori hilo la akiba. utakutana na vitu vitakavyokumbukumbusha historia uliyoisome shule ya msingi au sekondari kuhusu vita kuu ya kwanza ya dunia. huu mtambo upo ktk gate la Mtemere.

No comments:

Post a Comment