Thursday, January 14, 2010

Ukiwaona wapo wengi....

Basi ujue kuna roho ya mnyama imeonja mauti. Tai ni ndege ambao huishi kwa kula mizoga. wao hawana time ya kuinda, mishe mishe yao kubwa porini ni kuzengea mawindo ya wengine ili nao wapate kula pindi muwindaji anapotosheka.

mkiwa kwenye misele porini (game drive), hawa ndege wanakuwa na nafasi yao ktk misele yenu. mkiwaona wapo kwenye kongamano kama ilivyo hapo juu au wametanda angani, basi japo jaribu kusogea eneo karibu na walipo kwani unaweza bahatika kuona Sharubu, wa chini au hata wajuu wakipata mlo baada ya mawindo. ni nyenzo inayoweza kukusaidia kufanikisha azma ya kuwaona predators ktk hifadhi.

Hata bwana afya (fisi) pia huwa anafanikisha inshu zake za kupata msosi kwa kuzengea nyendo za tai, akiona kongomano lao tu anajua nae kashiba. Ki ukweli ukifuatilia mwenendo wa tai ukiwa porini unaweza ukaona mengi zaidi ya kile ulichotegemea.
[picha: Antelope Safaris]

No comments:

Post a Comment