Tuesday, January 19, 2010

Utalii wa Ndani - Pongo Safaris yaibuka na Chimbuko

kampuni ya Pongo Safaris mwaka jana ilijotosa ktk libeneke la utalii wa ndani nia ikiwa ni kuwapa nafasi wazalendo kutembelea na kuvijua kwa undani vivutio kadha wa kadha vya kitalii nchi yetu iliyobarikiwa navyo. Kampeni hii iliyopewa jina la Chimbuko Safaris ilizinduliwa rasmi mwaka jana ktk Uwanja wa kimataifa wa maonyesho ya kibiashara wa Mwl Nyerere (Al-maarufu kama saba-saba) na Waziri wa Utalii na Maliasili Mhe. Shamsa Mwangunga.

Uzinduzi huo ulienda sambamba na safari iliwapeleka wazelendo kadhaa ktk mji mkongwe wa bagamoyo ili kujifunza na kujionea mambo kadhaa huko. Uongozi wa Pongo unaahidi mambo kem kem kwa wazalendo wenye kupenda mambo ya kutembelea Vivution vy utalii zikiwemo mbuga za wanyama na maeneo muhimu ya historia ya nchi na mwanadamu kwa ujumla vilivyomo ndani ya Tanzania.


Miss Utalii wa ndani aka Domestic Tourism Sia Ndaskoi akila poz na moja ya ndinga za safari inayomilikiwa na Pongo Safaris ktk ofisi za pongo safaris.

No comments:

Post a Comment