Tuesday, January 19, 2010

Mount Meru game Sanctuary - Arusha, Usa river


Mount meru game sanctuary ipo njia ya Arusha-Moshi maeneo ya usa river, hapa kuna vyumba vya kulala sambamba na sanctuary ya wanyama kadhaa wa porini. ni mahali pazuri kutembelea na kupumzika uwapo Arusha. Juu ni vyumba vyao vya kulala wageni ambavyo vinatizamana na eneo waliopo wanyama - Sanctuary.

Aina mbali mbali za ndege wa porini nao wapo pia kuwakilisha

Mlima Kilimanjaro unakuwa unaonekana japo sio kwa urahisi sana lakini wenye lugha yao husema something is better than nothing. wakati huo (2007 zilipopigwa picha hizi) hali ya barafu mlimani ilikuwa si haba.

mto wa usa river wenyewe ndio huu, mto huu unapita kwa nyuma ya sanctuary.

Hapa kuna collection nzuri ya ndege mbali mbali. kwa mtu anaependa bird watching basi Mount Meru Game sanctuary ni sehemu murua kwenda kupumzikia.
Mbega (Colubus monkey) nao wapo kuwakilisha.


Wanyama wakubwa ambao ni wala nyasi nao wapo pia.

No comments:

Post a Comment