Wednesday, January 27, 2010

Ushirikiano ni nyenzo muhimu porini

Kuwa na guide ambaye anaijua hifadhi au pori ni nyenzo muhimu sana ili kuweza kufanikisha azma yako kama mgeni kuona wanyama na kujifunza mengi kuhusu wanyama wa porini na mazingira yao. inakuwa nzuri pale dereva anapokuwa anajua aende wapi ili kuona aina fulani ya mnyama au wanyama. na pia namna ya kufuata maelekezo atakayopewa na madereva wenzake kuhusu wapi mnyama mnaemtafuta ameonekana karibuni.

Ki ukweli wageni nao pia wanakuwa na nafasi ktk kufanikisha azma hii, kwani kuna vitu vingine guide anaweza asivione (kwa bahati mbaya) na mkawa mmevikosa. ktk hili, ushirikiano na guide ili ku-maximize uonekanaji wa wanyama ni muhimu sana. Mkiwa na guide mwerevu ataanza kuwapa hints na kuwsihi sana mumsimamishe au mmuulize pindi unapoona kitu ambacho si cha kawaida wakati mkiwa ktk game drive, guide wengi huwa na mwelekeo huu.

Siku moja tukiwa ktk misele ya porini ndani ya Hifadhi ya taifa ya Serengeti National park, tulifika mahali tukaona dalili za matairi ya magari mengine yakiwa yamekwenda hovyo hovyo na mengine yakiwa yamepita nje ya barabara. kwa wazoefu, hii ni ishara ya kwamba eneo hili kuna jambo ambalo ni vyema ukaliangalia kwani limewavutia wale waliokutangulia. Utakuta matairi yameenda ktk hali isiyo ya mstari ulionyooka.

baada ya kuona dalili hizi, guide alisimamisha gari na kusema tusaidiane kuangalia kila upande wa gari, juu na chini (kulikuwa na miti) ili kujua eneo hilo lina nini. Haukupita muda ambapo mmoja wa mgeni alipomuomba guide binocular (kiona mbali) kwani alihisi kwamba mmoja ya mti uliokuwa pembeni ulikuwa na kitu lakini kilikuwa kimejificha. baada ya kupewa binocular ndipo ilipodhihirika kwamba kitu hicho ni wajuu (chui) aliyekuwa amejipumzisha juu ya mti. Wajuu huyo alikuwa amekaa eneo ambalo kama si werevu na ushirikiano, ni dhahiri tungempita na tusingemuona.

Jambo hili linadhihirisha kwamba ushirikiano ni nyenzo muhimu inayoweza kukusaidi kuongeza nafasi za wewe kuona wanyama wengi na kujua mengi mengineyo. ukimwachia guide peke yake, basi wewe utaishia kuona anachokiona au kujua guide. ushirikiano na kuwa mdadisi kutakufanya uondoke porini ukiwa na uelewa mkubwa wa wanyama pori na mazingira yao.

No comments:

Post a Comment