Wednesday, January 27, 2010

Si simba wala chui.... ni kiboko


Kiboko ndie mnyama wa porini ambae anaelezwa kuwa anaongoza kwa kuuwa watu wengi barani Afrika kushinda mnyama mwingine yoyote wa porini. hii inatokana na hali ya hasira ambayo mnyama huyu anakuwa nayo awapo ktk himaya yake au hata nchi kavu.

hawa jamaa hawana utani pindi mtu anaposogea ktk himaya yake wanakuwa wakali zaidi endapo wakiwa na watoto wadogo ktk kundi lao. kiboko jike mwenye mtoto ni hatari sana ni vyema ukimkwepa mkiwa ktk boat ride. ukiwa Selous, pembezoni mwa mto rufiji utakutana na story za watu ambao mitumbwi yao ilipinduliwa na viboko pale ambapo waliingia ktk himaya zao bila kujua.

Kiboko kupendelea kuishi kwenye maji ni hii ni sababu nyingine inayompelekea kuuwa watu wengi hususan wale ambao hufanya shughuli zao ktk maziwa na mabwawa wanamoishi viboko au kufanya shughuli zao pembezoni mwa maziwa. Ugumu wa upatikanaji wa maji safi na salama hupelekea watu kujikuta wakifuata maji ktk maeneo ambayo yana viboko. hii inawaweka ktk hali ya hatari na kumfanya kiboko kuonekana ni mnyama mkali na muuaji kushinda simba na chui ambao huua kwa nia ya kupata mlo.

licha ya kwamba kiboko anaongoza kwa kuuwa watu, mauaji haya si kwa nia ya kupata kitoweo au mlo. Kiboko sio mla nyama, yeye ni mla nyasi kwa kwenda mbele. Vifo vyote vinaelezwa kuwa ni ktk sababu za kujihami zaidi na sio ktk kutafuta mlo. Hutumia meno yake makubwa ktk mashambulizi yake, hali ambayo wachache hutoka salama. picha zote ni Retima hippo pool Serengeti national park

No comments:

Post a Comment