Wednesday, January 27, 2010

Kisiwa cha Mnarani

Ukiwa unasafiri kwenda ZNZj kwa boat ukitokea Dar, moja ya ishara ya kwamba safari yako inakaribia kufika ukingoni ni kisiwa kilichozoeleka kama Mnarani. jina hili linatokana uwepo wa mnara unaotumika kuongozea meli. Katika kisiwa hiki pia kuna hoteli maarufu ambayo nayo imezoelekea kama mnarani, kufika ktk hiyo hoteli ni lazima uje kwa boat.

Sehemu ya hoteli ya Mnarani pamoja na Mnara wenyewe vikionekan toka ktk boat iliyokuwa ikielekea Zenj.

Kwa wengi ukisema Zanzibar basi umemaanisha ni muunganiko wa visiwa vya Unguja na Pemba. Zanzibar ni zaidi ya visiwa vya Unguja na Pemba, kwa taarifa yako tu, Zanzibar ni muunganiko wa visiwa 52 (vikiwemo Unguja na Pemba).
Unguja na Pemba ni visiwa vikubwa na vyenye wakazi wengi na shughuli nyingi za kibiashara zinapatikana ktk visiwa hii. zaidi ya hivi kuna visiwa kama vile Tumbatu (ambacho kinafuata kwa ukubwa na wingi wa watu baada ya kisiwa cha Pemba) Fundo, Kojani na vinginevyo vingi

Hivi sasa visiwa hivi vipo ktk mtihani kutokana na mjadala wa ukomo wa urais aliyeopo kuzua kambi kadhaa ktk ngazi za kiserikali na kichama. Shime ndugu zetu wa Visiwani msimame kidete na kufanya maamuzi mazuri na yenye mustakabali wa kitaifa ili kulinda amani na umoja ndani ya visiwa hivi tulivu. Tunapenda kuja tena na tena kuwatembelea na kujionea mandhari murua huko visiwani.

No comments:

Post a Comment