Kwa haraka haraka unaweza kusema kwamba huyo tembo anabisha hodi ili aingie ktk hiyo nyumba. Au ana-force kingi aingie kwa nguvu. lakini ukijulishwa ya kwamba hiyo nyumba imejengwa ndani ya hifadhi ya taifa ya Ruaha National park basi ni dhahiri utaweza sema kwamba huyo tembo hana haja ya kubisha hodi. Bali wakazi wa hiyo nyumba ndio inabidi wabishe hodi kila mara wanapotoka nje ya nyumba yao. Ki ukweli na kiuungwana kabisa, huyo tembo ndio mwenyeji wao na mazingira hayo ndio ndani mwake, yoyote anayeingia ktk mazingira yake, hana budi kufuata taratibu za tembo huyo na wakazi wengine wa maneo hayo. Zingatia hili na utaishi salama salmini na wanyama hawa hata kwa mwaka mzima, achia mbali game drive ya masaa kadhaa
picha juu imepigwa ndani ya hifadhi ya taifa ya Ruaha National park. hiyo ni nyumba ya wafanyakazi wanaoishio ndani ya hifadhi.
picha juu imepigwa ndani ya hifadhi ya taifa ya Ruaha National park. hiyo ni nyumba ya wafanyakazi wanaoishio ndani ya hifadhi.
No comments:
Post a Comment