Tuesday, January 12, 2010

Kisiwani - Same

Mwaka 2006 ikiwa ni ktk utekelezaji wa utaratibu wa ushirikiano na kufarijiana ktk ngazi ya ki-familia, nilijikuta nikiwa ktk convoy iliyokuwa ikelekea milima ya Upareni ya mbaga. Ili kufika huko milimani (kwa shemeji zangu) inakubidi upite sehemu moja inaitwa Kisiwani. taswira ya juu na chini ni picha chache nilizoweza kuzipiga tukiwa safari.
Unaweza kufika hapa kwa kuingilia Same au ukitokea Gonja. Kama utaingilia Same, safari yako hiyo itakupitisha ktk hifadhi ya taifa ya Mkomazi wakati unaelekea same.
mpaka sasa sijapata jibu kamili kwa nini kunaitwa kisiwani kwani sikuona mto au bwawa ambalo lingefanya eneo hilo kuwa Kisiwa kama nilivyozoea. mwenye kuelewa zaidi naomba atumwagie dondoo ktk hili


No comments:

Post a Comment