Ukiwa Crater view point na ikiwa ni mara yako wa kwanza kutembelea Ngorongoro crater, unaweza ukasema kimoyomoyo kuwa ni sehemu ya kuingia na kuspend a few minutes and you are done. si kweli... Hii sehemu kwa juu inaoneka na ndogo lakini ukiingia ina mambo ya kukustaajabisha na kukuburudisha. Ni sehemu ambayo ukipata guide anayeilewa na kuwaelewa wanyama vizuri, basi bila shaka safari yako ndani ya crater itadumu ktk fikra zako milele. Na jambo moja naomba uelewe, japo crater inaonekana ndogo na kama bakuli, lakini humo ndani kuna njia nyingi ambazo unaweza henya kutafuta pa kutokea. kwa taarifa yako tu, unapoingilia sipo ambapo utatokea. kuna njia mbili tofauti; crater descent na creater ascent routes. zingatia hili
Ukitia mguu utakutana na wanyama wa kila namna wakiendelea na shughuli zao za kila siku. Tofauti ninayo iona mimi kati ya mtu anaetembelea wanyama ktk zoo na yule anaeingia porini ni kwamba; Ukienda zoo, wanyama wanakuwa wamefungiwa ktk vyumba vyo na wewe mgeni unakuwa huru kwa kiasi fulani. Ilhali mtu akiingia porini kwenyewe, wanyama wanakuwa huru wakati wewe mgeni ndio unakuwa mfungwa ktk gari au chombo unachotumia. yote kwa yote, wanyama wa porini wanakuwa anakupa raha endapo utawaona wakiwa ktk mazingira yao ya kila siku - porini. Zoo, ziwe ni sehemu ya introduction tu ya wanyama wa porini.
Sharubu nao wapo kwa wingi tu. hii pride ni pride ambayo inajulikana, ukiingia crater na ukasema unataka kuona sharubu basi moja ya sehemu ambayo unaweza pelekwa na kuwabahatisha ni eneo linaitwa Korongo la John. huko utakutana na hii pride. Hapo tuliwakuta wakiwa wanatega mingo, kwa mbali kulikuwa na kundi la nyumbu napunda milia ambalo walikuwa wanalia timing wapate kitoweo
Ndani ya Crater hakuna hotel wala camping site. Shughuli zote za malazi ni nje ya crater, ukikutwa ndani ya crater usiku utakuwa na kazi ya kujieleza. Picha juu ilipigwa alfajiri toka Serena Ngorongoro, huwa kunakuwa na baridi na ukungu mzito kiasi cha kwamba crater inakuwa haionekani kabisa.
Muda ukizidi kwenda, jua hushika hatamu na taratibu crater inakuwa inaanza kuonekana toka hotelini. View ya crater ki ukweli inakuwa murua kwani unaiona toka ukiwa kitandani, kabla haujaamka.
Ukungu hupenya hadi sehemu nyingine za hotelini, hapa ni kwenye corridor iliyopo Serena Lodge, Ngorongoro.
No comments:
Post a Comment