Wednesday, January 27, 2010

Mayai ya Ndege wa porini

Hawa mayai yao yana rangi nyeupe. angalia eneo walilojenga viota vyao, miba kila kona

Ndege au hata wanyama wanaozaliana kwa kutaga mayai, huwa na namna inayofanana ya kuyaficha mayai yao ili yasidhurike kwa namna yoyote. Wapo ndege ambao hutumia muda mwingi kujenga na kuimarisha viota vyao. Ndege wengine hujenga viota vyao ktk miti mirefu sana au hata ktk miti ambayo in miiba mikali sana. wakati huo huo, wapo ndege ambao huyaacha mayai yao sehemu ambayo si ya kificho sana.

Inaelezwa kwamba kinachotofautisha mbinu za kulinda na kuyahifadhi salama mayai ni rangi ya yale mayai yenyewe. Ki ukweli, Ndege au mnyama ambaye mayai yake yana rangi nyeupe, hutumia nguvu zaidi ili kuyalinda mayai yake kwa kuwa yanaonekana kirahisi sana. Ndege au mnyama huyo hufikia hatua ya kujenga kiota ktk mti eneo ambalo ni mbali na waharibifu wa mayai yao - wanyama wengine, nyoka na hata binadamu. Mamba hujenga kiota chake nje ya maji lakini huhakikisha amekifukia vizuri na zaidi ya hapo huweka lindo madhubuti ili eneo husika lisisogelewe na mharibifu yoyote yule.

Wale ambao rangi ya mayai yao si nyeupe, wao huwa hawana wasiwasi sana wa kuyaficha mayai yao. wao watataga mayai yao sehemu ya wazi na kisha kuyaacha hapo bila ya kuchukua hatua za ziada kuyaficha. hii inatokana na imani yao kwamba si rahisi mayai yao kuonwa.

No comments:

Post a Comment