Saturday, January 9, 2010

Dondoo za kukwea mlima Kilimanjaro

kwa wanaokwea mlima kupitia route ya Marangu, shughuli huwa inaanzia hapa. Masaa unayoyaona (ETA) ni masaa ambayo mpandaji anategemewa kuyatumia kutooka point moja kwenda nyingine. kwa mfano wameandika Mandara 3Hrs, hiyo inamaanisha ni muda wa safari toka Marangu gate (hapo ilipopigwa picha) hadi Mandara.

Mzalendo wa kwanza kupanda Mlima akiwa kama guide wa mgeni (Hans Meyer).


Mambo muhimu ya kuzingatia ukiwa unapanda mlima Kilimanjaro

Soma notes vizuri ubaoni ili usije ukafeli mtihani wa kupanda mlima. Ni muhimu sana kuzingatia haya maelekezo kwani ikuyapuuza maisha yako yanaweza kuwa hatarini pia. Huu ni muongozo tu ili kukuwezesha mpandaji kufanikisha lengo lako la kupanda mlima hadi kileleni.

dondoo kuhusu viwalo vya kutinga wakati wa shughuli nzima ya kupanda mlima Kilimanjaro. Kutokuwa na viwalo isiwe kikwazo kwako, Marangu gate kuna wajasiriamali wanakodisha pamba mahususi kwa ajili ya kupandia mlima. Huna haja ya kununua au kusafiri na makoti yako kwa ajili ya kujilinda na baridi wakati wa kupanda mlima.


Wanaoendesha shughuli za kusindikiza wageni mlimani nao wana notes zao za kusoma na kuzingatia. Squad ya TembeaTz imeanza kujifua mdogo-mdogo ili nayo ijitupe ktk kinyang'anyiro cha kuukwea mlima Kili. Kaa chonjo mdau. [Picha - Friends of TembeaTz]

No comments:

Post a Comment