Wednesday, August 19, 2009

Game Walking Safaris... Selous Game reserve

wengi tumezoea kutembea mbugani ukiwa ndani ya gari maalum. Lakini ki-ukweli, kuna namna nyingi ambazo mtu anaweza tembelea mbuga na kujionea wanyama, mimea na mandhari ya eneo husika. kati ya hizi kuna Game walking (matembezi ya miguu) wengine hupenda kuuita trekking na hot air balloon safaris.
picha chini zinakuonyesha safari iliyofanywa na mtembezi ndani ya Selous Game reserve. ilikuwa ni safari ya kilometa 8 iliyoanzia geti la Mtemere na kuishia ktk moja ya maziwa mengi yaliyopo ktk pori hilo, Lake Mzizimia one (Ox-bow lake) Ni mwendo wa mstari kama wanafunzi wa shule ya msingi, huku guide mwenye bunduki akiongoza njia

Mnapokuwa njiani mnasimama na kupewa maelezo ya vitu mbali mbali mnavyokutana navyo. hapo juu guide anatoa maelezo ya mmea wa mkakati (Cactus plant). Tulipata maelezo pia kuhusu kwato na mwenendo wa wanyama ktk mbuga hiyo. utaona kwato mbali mbali za wanyama na jinsi ya kuweza kuzitofautisha

Guide mbele, wengine nyuma...

Sehemu nyingine mnazipita zinakuwa zinaogopesha lakini mwisho wa siku unatoka na uelewa mkubwa wa maisha ya wanyama na mazingira yao.


Gari likitungoja mwisho wa safari yetu, pembezoni mwa lake Mzizimia one
Mwisho wa game walk

No comments:

Post a Comment