Kituo cha Horombo, ni moja ya vituo ambavyo mgeni anakuwa anapata view nzuri ya jiji la Moshi, maeneo yake na baadhi ya vitu vilivyo ndani ya mkoa wa Kilimanjaro. Hali ya hewa ikiruhusu (hususan mawingu) ukiwa Horombo unauona mji wa Moshi vyema na usiku taa za jiji hilo zinaonekana vyema. Nyakati za usiku, taa za uwanja wa ndege wa Kilimanjaro huonekana na kama kuna ndege zinazoruka na kutua zinakuwa zinaonekana pia. Taa za maeneo ya Boma Ng'ombe na maeneo jirani huonekana pia. Picha juu ni mashamba ya miwa ya Kiwanda cha sukari cha TPC Moshi yakionekana.
Mashamba ya TPC yakionekana kwa mbali kidogo
Ziwa Jipe, ziwa hili lipo kwenye mpaka wa Tanzania na Kenya
Bwawa la Nyumba ya Mungu nalo linaonekana
Milima ya Upare nayo inaonekan hususan safu ya kaskazini
No comments:
Post a Comment