Baada ya kutembea kwa muda wa takriban masaa 8 kutokea kituo cha Mandara kuelekea Horombo, nilimsikia Guide wetu akitueleza kuwa "Tumeshafika Horombo, Mmeziona Huts?".. Awali hakuna kati yangu au Frank aliyekuwa na jibu kwani kipindi hicho huts zilikuwa hazionekani kabisa. Wingu lililoambatana na mvua lilitufanya tushindwe kuona mbali. Awali sote tuliona kama anatuzingua na kutupa moyo ili tuweze kuendelea na safari. Tulisimama kwa muda ili kunywa maji maana tulikuwa tumetoka kupanda kilima kikali kufika eneo hilo na ndipo ghafla tukaanza kuamini maneno ya guide kuwa tumeshafika Horombo Hut. Taratibu mawingu yalianza kupungua na mabanda yakaanza kuonekana. Sekunde chache kabla sijapiga picha ya juu, hata hilo daraja dogo linaloonekana upande wa Kushoto (chini) lilikuwa halionekani. Na wewe msomaji umeziona huts kwenye picha ya juu?
Kwa hapa unaweza ukaanza kuona baadhi ya huts (upande wa Kulia). Huts unazoziona ni huts ambazo zipo upande wa nyumba wa kituo cha Horombo. Hapa hali ya mawingu na mvua ikielekea kupungua na kuongeza uwezo wa kuona mbali
Bado wingu lilikuwa limetanda na huts zikionekana kwa mbali. Kati ya hapo tuliposimama na kilipo kituo cha Horombo kulikuwa na mto unapita na kufanya kuwa na korongo. Ili kufika Horombo inkubidi uvuke Daraja linaloonekana kwenye picha ya awali ya post hii.
No comments:
Post a Comment