Kwa tulio wengi, tunaposikia utalii moja kwa moja huwa tunahusisha vivutio mbalimbali asilia ambavyo nchi inakwa nayo. Hifadhi za taifa, mbuga za wanyama, Milima, Mabonde, mito na kadhalika. Mara nyingi kipengele cha mila na utamaduni huwa hakiingizwi kwenye mlinganyo wetu. Hii huchochewa na hali ya wengi kuhamasishwa zaidi na mandhari za maeneo yenye vivutio au wanyama waliopo na kuona mambo ya utamaduni kama sio ya msingi. Huu si mtizamo sahihi na ni mtizamo ambao wengi wetu inabidi tuufute. Mila, Desturi na utamaduni wa jamii mbalimbali ni kichecheo muhimu kwa utalii. Hivi sasa wageni wengi huweka siku moja ua zaidi ambapo hupenda kutembelea jamii na kujifunza jinsi inavyoishi na kukabiliana na changamoto zake. Utamaduni wa namna hii umeshamiri zaidi kwenye ukanda wa kaskazini ambapo makabila ya Wamaasai, Wahadzabe na Watindiga wamekuwa kivutio kutokana na wao kulinda na kudumisha mila zao za enzi na enzi mpaka sasa. Kabila la Wamaasai mpaka sasa linadumisha mila zake mbalimbali kama vile jando, utegemezi wa mifugo yao kwenye maisha na mambo mengine. Wahdzabe mpaka sasa wao wanaendelea na mfumo wao wa maisha ya kuokoteza vyakula porini na uwindaji wakati Watindiga nao hawatofautiani sana na Wahadzabe. Hivi karibuni, mdau Thomas wa HSK Safaris alielekea kwenye vijiji vilivyopo karibu na ziwa Eyasi ili kuwapeleka wageni aliokuwa nao kujionea maisha ya jamii zinazoishi maeneo hayo. Picha Juu ni Mdau Thomas akiwa na familia moja walioyoitembelea kwenye boma yako huko Eyasi.
Moja ya boma zilizopo huko.
Picha zote na Mdau Thomas wa HSK safaris
No comments:
Post a Comment