Kipindi cha
Kambi Popote kinachorushwa Clouds Tv kitaungana na Lakeland Africa kwenye
safari ya siku 14 za ‘Mtanzania tembelea Tanzania’ amabyo itaanza
desemba 14 mwaka huu na kumalizika desemba 27 mwaka huu.
Mtangazaji
wa kipindi hiki Antonio Nugaz ataiongoza timu yake nzima katika safari hii ya
kuvutia huku timu yote kwa ujumla ikipata huduma ya tour guide maarufu kutoka
Lakeland Africa mwenye uzoefu wa miaka zaidi ya 3o katika sekta ya utalii.
Safari hii
itaanzia Dar es Salaam, na kupita katika hifadhi za Sadan, Pangani, Lushoto,
Tarangire, Olduvai Gorge, Ziwa Manyara, Ngorongoro Crater, Hifadhi ya Serengeti
na itahitimishwa Butiama kwa Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.
Watanzania
watakaosafiri na Kampuni ya Lakeland Africa katika safari hii ya siku 14 za ‘Mtanzania
tembelea Tanzania’ watapata huduma safi ndani ya lori la kitalii wakiwa
safarini ikiwemo kila mtalii kuwa na soketi yake ya kuchajia simu, laptop na
kamera.
Pia kila
mtalii atakuwa na kabati lake dogo (locker) kwa ajili ya kufungia vitu vyake
vya thamani kama vile passport, vitambulisho na kwamba kila mtalii anatakiwa
kuja na kufuli lake la kufungia kabati lake.
Mbali na
hayo kila mtalii atakuwa na taa yake ya kusomea wakati wa usiku, gari lina
tanki la maji lenye ujazo wa lita 500 na kila mtalii atapewa lita 20 kwa siku
na kwamba kutakuwa na firiji ya vinywani baridi na vitu vinavyoharibika.
Kwa
mawasiliano na Lakeland Africa
+255222-761811
+255784885901
‘Kuwa mtalii
ndani ya nchi yako’
No comments:
Post a Comment