Wednesday, May 30, 2012

Walitega mtego wao pembezoni ya mto Ruaha....

Ni Kundi kubwa la Sharubu jike ambalo lilikuwa sambamba na Dume moja. Simba hawa kwa kubaini kuwa wanyama huitaji maji ya kunywa mara kwa mara, walitega mtego wao pembezoni mwa mto Ruaha ili waweze kumnasa yoyote atakayekatiza maeneo hayo kuelekea Mtoni. Siku hii mtego wao ulijibu kwani walifanikiwa kukamata mnyama aliyewatoa kwenye njaa

Waswahili husema Mungu hamtupi mja wake, na sharaubu hawa waliweza kukama mnyama aliyewapa lishe ya kutosha kwa siku hiyo. Hapo walikuwa wamua Twiga aka Mrefu.

Baadhi ya sharubu wakiendelea kumalizia windo

Japo jike ndiye muwindaji, Dume ndie msimazi wa zoezi la kula. Kama kuna dume karibu, sharubu jike hawaanzi kula mpaka dume aje kuzindua. Dume hili lilikuwa pembeni ya kundi la majike ambao walikuwa wakiendelea kukwangua nyama zilizobakia kwenye windo lao. 
Picha zote na Mdau Rajab wa Wildness Safaris

No comments:

Post a Comment