Kufuatia vitendo vya vurugu zilizozuka hivi karibuni katika maeneo
kadhaa ya Mji wa Zanzibar baada ya mitandao ya kimataifa imekuwa
ikiripoti taarifa za kuwepo kwa hali ya wasiwasi kwa watalii wanaotaka
kuja kutembelea Visiwa hivyo.
Kama Waziri mwenye dhamana ya masuala ya Utalii, ningependa
kuwahakikishia wageni, ambao tayari wako nchini, na wale ambao
wanajiandaa kuja, kuwa vurugu hizo ambazo zimeshadhibitiwa na Serikali
hazikuathiri utalii. Mjini Zanzibar pamoja na maeneo ya vivutio vya
utalii kote nchini.
Hadi hivi leo napotoa taarifa hii, amani imetawala Mji Mkongwe
Zanzibar na hakuna taarifa yoyote ya uharibifu wa maeneo ya vivutio vya
utalii vya Zanzibar wala kuchomwa kwa hoteli ama kudhulika kwa raia
yeyote wa kigeni. Hivyo nasisitiza kuwa Zanzibar nisehemu salama kwa
watalii.
Vilevile, Siku chache kabla ya tukio la Zanzibar, kulikuwa na matukio
manne ya watalii kuporwa katika maeneo ya Masaki jijini Dar es Salaam.
Uporaji huo ulitendwa na watu waliokuwa kwenye magari au pikipiki ambao
waliwapora watembea kwa miguu.
Serikali inawahakikishia wananchi na jumuiya ya kimataifa kuwa hayo
yalikuwa matukio ya pekee na ya kimataifa kuwa hayo yalikuwa matukio ya
pekee na ya kupita na hatua zimechukuliwa na Jeshi la Polisi kuongoza
usalam kwa wakazi na watalii.
Nachukua fursa hii kuwahakikishia wageni kwamba kila juhudi
zimechukuliwa kuhakikisha kuwa usalama wa watalii unadumishwa pamoja na
faraja wakati watakapotembelea Tanzania.
Daima tukumbuke kuwa, Tanzania ni kisiwa cha amani na nchi imenuia kidumisha sifa hiyo nzuri
Mhe. Lazaro Nyalandu
NAIBU WAZIRI
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII
30 Mei, 2012
No comments:
Post a Comment