Sunday, August 21, 2011

Utafanya nini?

Upo ndani ya hifadhi kwenye game drive na ghafla mnakutana na jamaa kajaa barabarani kama umuonavyo ktk taswira ya hapo juu. Wewe unataka uendelee na safari yako (tena kwa usalama), utachukua hatua gani ili mambo yaende sawa bin sawia? Kumbuka ya kwamba porini hakuna mambo ya honi na masikio ndio hawapendi kabisaa makelele yasiyokuwa na mpango. Mdau Tom wa Kimasafaris alikumbana na huyu masikio wiki iliyopita alipokuwa ndani ya hifadhi ya Mikumi.
Picha - mdau Tom wa Kima Safaris

No comments:

Post a Comment