Friday, August 19, 2011

Barabara ya Arusha-Babati mpaka Dodoma

Barabara ya Arusha-Babati mpaka Dodoma ni moja ya barabara muhimu kwa mkoa 'mpya' wa Manyara. Ni moja ya barabara inayouunganisha mkoa wa Manyara na Arusha na pia mkoa wa Manyara na Dodoma. Kwa kipindi kirefu barabara hii imekuwa ipo chini ya ukarabati. Hivi karibuni mdau Sam Diah wa Tanzania Travel company alikuwa na pilika pilika zilizompitisha katika barabara hii na zifuatazo ni baadhi ya taswira alizoweza kuzinasa akiwa njiani. Juu ni vifaa vya ujenzi zikiendelea na kazi katika barabara hii. Kwa wale waliowahi kufanya safari ktk barabara hii watakuwa na kumbukumbu nzuri za vumbi zito linalofunika gari kabisa hususan kipindi cha kiangazi ktk maeneo ambayo ujenzi ulikuwa haujakamilika.

Baadhi ya sehemu barabara imekamilika. Milima inayoonekana kwa mbali ni milima ya Hanang. Kwa wale waliowahi tembelea hifadhi ya Taifa ya Tarangire kwa njia ya gari. walitumia barabara hii kufika hifadhini

Barabara huharakisha maendeleo mengina. picha ni mjengo wa shule

Moja ya madaraja yalipo ktk barabara hii. hili lipo maeneo ya Dareda
Picha kwa hisani ya mdau Sam Diah wa Tanzania Travel Company

No comments:

Post a Comment