Lengo lilikuwa ni kufanya matembezi kwenye pwani ya raskutani asubuhi na mapema wakati jua likichomoza. azma ikiwa ni kupata taswira ya mawio (jua kuchomoza). Kwa bahati mbaya sana breki za usingizi zilishindwa kufanya kazi asubuhi hii na kupelekea kupitiliza mpaka wakati jua likiwa limeshashika hatamu. uchelewaji huu haukusitisha zoezi la matembezi kwenye pwani ya hotel ya ras Kutani. Picha juu ni sehemu ya maakuli ya hoteli inavyoonekana tokea ufukweni.
Hii sehemu nimeipenda sana. Ningependa kuitembelea. Ningepata mawasiliano ya hili eneo ili nijue gharama na jinsi ya kufika hapo. Panaonekana ni tulivu sana tofauti na beach nyingi kama coco na nyinginezo
ReplyDeleteJSK,
ReplyDeleteHii hotel wana utaratibu wa kutaka kila mgeni wao kufanya booking kabla ya kuwatembelea. kwenye moja ya mitundiko nimetoa link ya website yao ambayo wana sehemu ya kufanyia booking. Peruzi tovuti yao ujue zaidi au wasiliana na tour operator uliye karibu nae akufanyie mpango
Ni beach iliyotulia sana
Nafahamu hiyo ni private beach,hivi wanaruhusu watu kwenda au ni lazima uwe umefanya booking ya kulala hapo?
ReplyDelete