Hizi ni picha zilizochorwa na msanii kuonyesha mandhari ya Hotel ya Mount Meru itakavyokuwa pindi ujenzi utakapokamilika na kufungua milango yake kwa wageni. Hoteli hii iliyopata kuvuma miaka ya themanini na mwanzoni mwa miaka ya tisini inatarajia kufunguliwa rasmi mnamo mwezi Novemba mwaka huu. Itarudi tena ikiwa ktk hadhi ya nyota 5 na kuahidi ushindani mkubwa ktk sekta ya huduma za malazi ktk miji ya Arusha na Moshi.
http://www.mountmeruhotel.com/
Unaweza kutembelea tovuti ya hotel hii na kujionea hatua zinazoendelea ktk ujenzi na pia kupata taaraifa zaidi. ktk sehemu ya news, kuna maelekezo kwa wadau ambao wangependa kujaribu bahati zao ktk kinyang'anyiro cha ajira ktk hotel hii. Shukran sana kwa Mdau Bonny toka Karibu Fair Arusha kwa kutuhabarisha mambo haya na mengine mengi.
nimependa safi sana
ReplyDelete