Monday, August 23, 2010

Uwoga

Mdau, utakuwa tayari kufanya safari ndani ya hifadhi ukiwa ndani ya gari kama uionayo ktk taswira ya juu?

Kuna mtu aliiona hii picha akasema kwa jinsi alivyo muoga ktk mambo ya porini, kamwe hataweza kuthubutu kwenda porini ktk gari la wazi kama hilo. Hunishangaa mie natoa wapi ubavu wa kuliacha gari na kisha kutembea kwa miguu kilomita na masaa kadhaa ndani ya hifadhi yenye wanyama wakali. Naomba kujua, kuna wengine wenye uwoga kama wa mdau huyu ambae kwa leo namhifadhi jina lake?

3 comments:

  1. NDUGU YANGU MIMI MWENYEWE SIWEZI THUBUTU KWENDA PORINI KUTUMIA GARI YA NAMNA HIYO HATA KWA KULIPWA. LABDA HAPA TUAMBIANE UKWELI NI KWANINI NISIOGOPE KUSAFIRI PORINI NA GARI KAMA HIYO?. NAOMBA MAELEZO PLEASE MAANA HAKUNA MTU ALIYE WAHI KUNIPA MAELEZO YA KISAYANSI, KILA ANAYE NIELEZA KUHUSU PORINI/WANYAMA WAKALI ANATOA MAELEZO YAKE KIUZOEFU ZAIDI NA SIYO KISAYANSI. PLZ NAOMBA MAELEZO AU MAKALA ZINAZOELEZEA TABIA ZA WANYAMA WAKALI DHIDI YA BINADAAM

    ReplyDelete
  2. gari la namna hii mimi siliwezi hata kidogo. Heri yenu wenye ubavu wa kulimudu na hata kutembea ndani ya national park

    ReplyDelete