Tuesday, July 13, 2010

Vinasaidia, lakini...

Havitakuwezesha kujua kwa uhakika wapi uende ili kuona mnyama ambae ungependa kumuona siku hiyo ili kujua zaidi...

Hifadhi nyingi za hapa Tanzania (hata mapori ya akiba) yamewekewa vibao ambavyo vinakuonyesha upo wapi, unaelekea wapi na cha muhimu zaidi kukuonyesha wapi lilipo gate la kutokea/kuingilia ktk hifadhi. jambo moja ambalo vinaweza visiwe na msaada kwako ni kujua wapi uende ili kuona unachotaka kuona siku hiyo. Hapo ndio uzoefu na ushirikiano na wengine unapokuwa muhimu. Itakulazimu kuuliza getini unapoingia ktk hifadhi ili wakuambie wapi uelekee kuona nini au uulize madereva na wageni wangine unaokutana nao ukiwa ktk mizunguko yako wakueleze wameona/kusikia nini huko walikotoka. Kama sio mzoefu wa hifadhi, ukiwa na ramani ya hifadhi mkononi unaweza zunguka bila ya kuwa na wasiwasi wa kupotea ndani ya hifadhi. Ramani za barabara za hifadhi zinakuwa zinauzwa getini.

No comments:

Post a Comment