Thursday, July 29, 2010

Usione vyaelea - Karibu fair

Ni taswira ambazo TembeaTz imezipata toka kwa mdau wa Karibu fair zikionyesha hatua za awali za maandalizi ya maonesho ya karibu aka karibu fair ambayo yalifanyika mwezi Juni mwaka huu, nje kidogo ya jiji la Arusha.

Ni maonesho ambayo huleta pamoja wadau mbalimbali ktk sekta ya utalii huku kila mmoja akionyesha bidhaa na shughuli zake ktk sekta. hutoa fursa kwa wadau ktk sekta kukutana na kubadilishana mawazo.

Maonesho haya hufanyika ktk viwanja vya magereza, vilivyopo ktk barabara ya Arusha-Dodoma. TembeaTz inawapongeza waandaji kwa kazi nzuri, na kila la kheri ktk maandalizi ya show ijayo.

www.karibufair.com

No comments:

Post a Comment