Friday, July 30, 2010

Ngongongare Nature Trail - Arusha National Park

Ni mfumo wa mapito kwa ajili ya mgeni atakayependa kufanya walking safari kuanzia geti la Ngongongare ktk hifadhi ya taifa ya Arusha. kwa hifadhi ya Arusha, mgeni anaweza kufanya walking safari aidha kwa kuanzia geti la ngongongare au geti jingine lijulikanalo kama Momella gate. Kwa wale watakaochagua kuanzia Ngongongare gate basi watatumia njia hii mahususi kwa zoezi hili.

Baadhi ya ndondoo kuhusu mapito haya. Bango hili lipo pembezoni mwa eneo la kuegeshea magari pembezoni mwa geti la Ngongongare ktk hifadhi ya Taifa ya Arusha.

Mafuvu ya baadhi ya wanyama yakiwa juu ya kibao elekezi sambamba na tunda toka ktk M-Sausage tree. Hiyo ndio sausage yenyewe (mwisho kulia).

No comments:

Post a Comment