Thursday, July 29, 2010

Mateja wa Arusha NP

Tukiwa njiani kuelekea Ngurdoto crater tulikuta kundi la nyani aka mateja wakiwa wamefunga mtaa huku wakivinjari barabarani. Mmoja ndio alikuwa kalala chali, full kujiachia

Hapa sijui alikuwa anafanya yale mazoezi ya kukata tumbo au la!

Kwakuwa porini hutakiwi kupiga honi au kuwabugudhi wanyama ilibidi tuwe wapole tusubiri mpaka watakapoondoa kizuizi chao ndio nasi tuendelee na safari zetu.

Kwa bahati nzuri kulitokea sauti toka porini ambayo iliwashtua kundi lililokuwa barabarani na kuwafanya waache kula siesta na kuanza kuingia mitini. Hali hii ilitupa fursa ya kuendelea na safari yetu japo tulikuwa tunafurahia vituko vyao muda walipokuwa hapo barabarani.

No comments:

Post a Comment